Tija za tohara kwa jamii za Kiafrika: Uchunguzi wa mhusika Omolo katika riwaya ya ua la faraja (2004)

dc.contributor.authorFuluge, Adria
dc.contributor.authorDuwe, Martina
dc.date.accessioned2026-07-13T06:56:42Z
dc.date.issued2025
dc.descriptionPaper submitted to the" Journal of Kiswahili and Other African Languages" for publication
dc.description.abstractKatika jamii nyingi za Kiafrika, tohara ni mchakato wenye thamani na tija kubwa kwa baadhi ya makabila, husuani kwa kijana wa kiume. Katika makabila hayo, asiyetahiriwa huonekana kuwa bado ni mtoto na hajakomaa kifikra na kiutu, ambapo huweza hata kutengwa katika kushirikishwa baadhi ya masuala ya kijamii. Kijana huyo kama umri wake ni mkubwa, huweza kudharauliwa na rika lake na hata waliopo chini yake. Sambamba na hilo, katika maisha halisi ya Waafrika, tohara huchukuliwa kwa thamani inayoweza kuendeleza na kuhifadhi utambulisho wa kitamaduni na kijamii. Kwao, tohara humfanya mtu atambulike kwa namna tofauti na ilivyokuwa awali. Kwa jumla, thamani ya tohara kwa Waafrika ni suala lililowashughulisha wataalamu wengi. Hata hivyo, pamoja na kuwepo kwa tafiti nyingi kuhusu tohara kwa Waafrika, bado tija za tohara kwa kufungamanisha na fasihi andishi haijamakinikiwa kwa umahususi wake. Kwa hiyo, makala hii inashughulikia jambo hilo kwa kumrejelea mhusika Omolo kutoka riwaya ya Ua la Faraja (2004). Data za matokeo haya zilipatikana maktabani kwa kutumia mbinu ya usomaji matini. Vilevile, misingi ya Nadharia ya Sosholojia ya Kifasihi imetumika katika mchakato wa kuchunguza, kuchanganua, na kuwasilisha data zilizozaa matokeo hayo. Mjadala unaonesha kwamba tohara katika maisha ya Waafrika ina tija mbalimbali kulingana na utoshelevu wa kaida zao. Makala hii inajadili tija nne; nazo ni: Kudumisha mila, kuleta heshima kwa mhusika, kujikinga na magonjwa, na kujenga ujasiri na ukakamavu.
dc.description.sponsorshipPrivate
dc.identifier.citationAPA
dc.identifier.issn(Online): 2958-4914
dc.identifier.urihttps://doi.org/10.58721/jkal.v3i2.1413
dc.identifier.urihttps://scholar.mzumbe.ac.tz/handle/123456789/2185
dc.language.isoen
dc.publisherJournal of Kiswahili and Other African Languages
dc.subjectTohara — Afrika
dc.subjectTohara — Vipengele vya kijamii
dc.subjectFasihi ya Kiswahili — Historia na uhakiki
dc.subjectRiwaya ya Kiswahili — Historia na uhakiki
dc.subjectWahusika na sifa zao katika fasihi
dc.subjectSosholojia ya fasihi
dc.subjectFasihi na jamii
dc.subjectAfrika — Mila na desturi.
dc.subjectCircumcision — Africa
dc.subjectCircumcision — Social aspects
dc.subjectSwahili literature — History and criticism
dc.subjectSwahili fiction — History and criticism
dc.subjectCharacters and characteristics in literature
dc.subjectSociology of literature
dc.subjectLiterature and society
dc.subjectAfrica — Social life and customs
dc.titleTija za tohara kwa jamii za Kiafrika: Uchunguzi wa mhusika Omolo katika riwaya ya ua la faraja (2004)
dc.typeArticle

Files

Original bundle

Now showing 1 - 1 of 1
Thumbnail Image
Name:
Fuluge, A. and Duwe, M.- (2025).pdf
Size:
260.19 KB
Format:
Adobe Portable Document Format

License bundle

Now showing 1 - 1 of 1
No Thumbnail Available
Name:
license.txt
Size:
1.71 KB
Format:
Item-specific license agreed to upon submission
Description:

Collections